-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Vimanda vya viazi vya kuponda, ni kitafunio kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia kiazi mviringo kilicho chemshwa na kupondwa, mayai, vitunguu maji, pamoja na viungo. Kitafunio hiki chafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, pamoja na kinywaji chochote ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika vimanda hivi vya viazi vya kuponda.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria dogo. Weka kwenye hilo sufuria kiazi mviringo, chumvi kiasi, pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona kimeiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na kiazi peke yake, kisha acha kipoe.
Menya maganda ya kiazi hicho, kisha kiponde vizuri.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, kiazi ulichokiponda, mayai, vitunguu maji, ¼ kikombe cha majani ya giligilani, tangawizi, chumvi, pamoja na pilipili manga, kisha changanya vizuri.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mchanganyiko wa mayai uliochanganya, kisha funika kikaango na ukaange kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona upande wa chini wa mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. (Weka mchanganyiko huo wa mayai kwa awamu 2 mpaka 3)
Nyunyizia ¼ kikombe cha majani ya giligilani yaliyobaki juu ya huo mchanganyiko wa mayai, kisha kandamiza taratibu majani hayo kwa kutumia kijiko cha kukaangia (spatula) ili yashikane vizuri na mchanganyiko wa mayai.
Chukua sahani kubwa. Weka sahani hiyo ndani ya kikaango, kisha pindua kikaango juu chini ili kimanda kipate kigeuka na kuhamia kwenye sahani.
Telezesha kimanda kwenye kikaango, halafu rudisha kikaango kwenye jiko, kisha kaanga upande wa pili wa kimanda hicho kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona na upande huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Kunja kimanda katikati, kisha ondoa kwenye kikaango na ukiweke kwenye sahani, tayari kwa kula. Rudia hatua ya 5 mpaka 9, kwa mchanganyiko wa vimanda uliobaki.
Leave a Review