Jarida la Mapishi

Biskuti za nazi

 • Maandalizi
  Saa 1 Dk. 45
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  20

Biskuti za nazi, ni biskuti tamu, ambazo zinapikwa kwa kutumia unga wa ngano, nazi, siagi pamoja na sukari. Buskuti hizi sio tu ni tamu, bali pia ni rahisi kupika. Unaweza kupika biskuti hizi kwa muda mfupi wa dakika 15 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, sukari, pamoja na coconut extract, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka yai na uchanganye vizuri, kisha weka unga wa ngano, chumvi, nazi, na baking powder, halafu changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko wako umechanganyika vizuri na kupata donge kubwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kuchanganyia na uweke kwenye bakuli kubwa safi, kisha funika bakuli hilo kwa kutumia plastic wrap na uweke kwenye friji kwa muda wa dakika 30.

  Step3

  Baada ya dakika 30, ondoa bakuli lenye donge la biskuti kwenye friji, kisha chukua kibao cha kusukumia chapati na ukipake unga wa ngano. Kata kipande cha donge na ukifinyange vizuri na kupata umbo la mpira. Weka kipande hicho cha donge juu ya kibao cha kusukuma chapati na usukume hadi utakapo ona kipande hicho cha donge kimenyooka na kuwa kama chapati. Tumia glasi ya bati kukata biskuti katika umbo la duara, au kifaa chochote cha kukatia biskuti ulicho nacho cha umbo lolote upendalo. Rudia hatua hii hadi donge lote litakapoisha.

  Step4

  Chukua biskuti ulizozikata na uzipange kwenge sinia la kuoka (baking sheet). Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *