Jarida la Mapishi

Biskuti za maboga na machungwa

 • Maandalizi
  Dakika 45
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  20

Biskuti za maboga na machungwa, ni biskuti ambazo hupikwa kwa kutumia boga lililo sagwa, machungwa yaliyo kamuliwa, maganda ya machungwa yaliyo kunwa, pamoja na viungo. Biskuti hizi zafaa sana kula katika msimu wa vuli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za maboga na machungwa.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na powdered sugar, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka maganda ya chungwa yaliyo kunwa, chungwa lililo kamuliwa na boga, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, unga wa lozi, chumvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *