-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji4
Mahindi ya kuchoma, ni kitafunio kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kuyachoma mahindi kwenye jiko la kuchomea, kisha kuyapaka limao pamoja na viungo. Mahindi haya yafaa kula yenyewe kama yalivyo, hasa katika msimu wa baridi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mahindi haya ya kuchoma.
Ingredients
Directions
Washa jiko la kuchomea mahindi, kisha acha jiko lipate moto. Weka mahindi juu ya hilo jiko, kisha choma huku ukiyageuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Chukua sahani ndogo. Weka Chaat Masala kwenye hiyo sahani.
Chukua kipande kimoja cha limao halafu chovya kwenye Chaat Masala, kisha paka kwenye mahindi unayoyachoma, hadi utakapo ona mahindi yote yameenea vyema mchanganyiko huo wa Chaat Masala na limao. Ondoa mahindi hayo kwenye jiko la kuchomea na uyaweke pembeni kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review