Jarida la Mapishi

Biskuti za shayiri na chocolate

 • Maandalizi
  Saa 1
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  30

Biskuti za shayiri na chocolate, ni biskuti tamu na laini, ambazo hupikwa kwa kutumia unga wa ngano, shayiri, pamoja na dark chocolate chips. Biskuti hizi zafaa sana kula kama kitafunio cha kawaida pamoja na glasi ya maziwa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za shayiri na chocolate.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria ndogo. Weka siagi kwenye hilo sufuria, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, halafu acha siagi iyeyuke.

  Step2

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi uliyo iyeyusha, pamoja na light brown sugar, kisha changanya vizuri.

  Step3

  Weka yai na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.

  Step4

  Weka shayiri, unga wa ngano, baking soda, chumvi, pamoja na dark chocolate chips, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step5

  Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

  Step6

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step7

  Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *