Jarida la Mapishi

Supu ya mtindi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Supu ya mtindi, ni supu nzuri na rahisi kupika inayofaa kunywa katika misimu ya vipindi vyoye vya mwaka. Supu hii husaidia kuongeza joto mwilini katika majira ya baridi, lakini pia husaidia kuleta baridi mwilini katika majira ya joto. Waweza kunywa supu hii pamoja na chakula chochote ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ukifunze jinsi ya kupika supu hii ya mtindi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango mchele, choroko, mbaazi, pamoja na mbegu za binzari nyembamba, kisha kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara bila kutumia mafuta kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni.

  Step3

  Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, mtindi, maji, tangawizi, pamoja na vitunguu swaumu, kisha saga vizuri. Weka binzari ya manjano, chumvi, pamoja na mchanganyiko ulio usaga mwanzoni, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko wote umesagika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia, na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga vizuri.

  Step5

  Weka mchanganyiko wote ulio usaga, kisha acha ichemke katika jiko lenye moto mkubwa huku ukikoroga mara kwa mara. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10.

  Step6

  Weka majani ya giligilani na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kula.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *