Jarida la Mapishi

Supu ya njegere

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Supu ya njegere, ni supu tamu yenye rangi ya kijani na rahisi kupika, ambayo yafaa kunywa katika msimu wa baridi. Supu hii hupikwa kwa kutumia njegere mbichi, mtindi, pamoja na viungo. Waweza kunywa supu hii pamoja na mkate au wali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya njegere.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, njegere pamoja na vikombe 2 vya maji, kisha weka hilo sufuria kwenye jiko lenye moto mkubwa halafu acha ichemke.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20 au hadi utakapo ona njegere zimeiva. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, njegere ulizo zichemsha, kisha saga hadi utakapo ona njegere zimesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa njegere hizo kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uziweke pembeni kwenye kontena.

  Step4

  Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, mtindi, unga wa mahindi pamoja na kikombe 1 cha maji, kisha saga vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step5

  Weka tena kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, tangawizi pamoja na vitunguu swaumu na usage hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step6

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga, kisha kaanga kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step7

  Weka mbegu za giligilani pamoja na binzari nyembamba na ukoroge vizuri. Weka njegere ulizo zisaga, chumvi, pamoja na vikombe 3 vya maji vilivyobaki, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na acha ichemke katika moto mkubwa.

  Step8

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10.

  Step9

  Weka mchanganyiko wa mtindi ulio usaga na ukoroge vizuri, vizuri kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 3 zaidi.

  Step10

  Weka pilipili manga na ukoroge vizuri, kisha epua supu na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kunywa.

  Conclusion

  Kabla ya kuutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *