Jarida la Mapishi

Supu ya buttermilk

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  4

Supu ya buttermilk, supu yenye virutubisho vingi inayofaa kunywa katika kipindi cha kiangazi. Supu hii hupikwa kwa kutumia maziwa ya buttermilk pamoja na viungo. Unaweza kuinywa supu hii yenyewe kama ilivyo, au pamoja na wali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya buttermilk.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria ndogo yenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, dengu, mbegu za giligilani, mbegu za uwatu, pamoja na mbegu za pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona dengu zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.

  Step2

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko ulio ukaanga pamoja na ¼ kikombe cha maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanyanyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mbaazi, vikombe 3 vya maji, nyanya, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step4

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona mbaazi zimeiva.

  Step5

  Weka majani ya giligilani pamoja na mchanganyiko ulio usaga halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi.

  Step6

  Chukua sufuria ndogo yenye kijiko 1 cha chai cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, binzari nyembamba, pamoja na majani ya mvuje, halafu kaanga vizuri, kisha epua mchanganyiko huo na umimine kwenye supu.

  Step7

  Weka kwenye hiyo supu buttermilk pamoja na vitunguu vya kijani, kisha koroga vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *