Jarida la Mapishi

Supu ya nazi

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Supu ya nazi, ni supu nzuri na rahisi sana kupika ambayo hupikwa kwa kutumia tui la nazi. Ukiachana na nazi, supu hii huwekewa viungo mbali mbali kama vile, binzari nyembamba, mbegu za haradali, n.k, ambavyo huifanya supu hii tamu na yenye ladha ya kipekee zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika supu hii ya nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka vikombe 2 vya maji, kisha roweka mbaazi ndani ya hilo bakuli lenye maji, kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Baada ya dakika 30, mimina mbaazi ulizo ziroweka kwenye sufuria la kubwa pamoja na maji uliyotumia kuroweka hizo mbaazi. Weka pia kwenye hilo sufuria, binzari ya manjano, chumvi, pamoja na kikombe 1 cha maji, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto mkubwa, halafu acha ichemke.

  Step3

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona mbaazi zimeiva. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step4

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko wa mbaazi ulio chemsha kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step5

  Chukua sufuria nyingine kubwa yenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mbegu za haradali, binzari nyembamba, pilipili manga, majani ya mvuje, pamoja na nazi iliyo kunwa, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step6

  Weka nyanya, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara, kwa muda wa dakika 2.

  Step7

  Weka Tamarind Paste pamoja na vikombe 2 vya maji vilivyobakia, kisha acha ichemke katika moto mkubwa. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha acha indelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva na kuwa laini.

  Step8

  Mimina mchanganyiko wa mbaazi ulio usaga na ukoroge vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.

  Step9

  Weka tui la nazi pamoja na majani ya giligilani na ukoroge vizuri, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 2 zaidi, kisha epua na upakue kwenye bakuli, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *