Jarida la Mapishi

Pilau ya dengu

Pilau ya dengu | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Pilau ya dengu, ni chakula kizuri ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, vitungu maji, dengu zilizo chemshwa, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya dengu.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki pamoja na mdalasini, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step3

    Weka binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step4

    Weka tangawizi, vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

    Step5

    Weka nyanya pamoja na dengu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step6

    Weka mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step7

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step8

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.