Jarida la Mapishi

Pilau ya nazi

Pilau ya nazi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Pilau ya nazi, ni pilau nzuri ambayo yafaa kula pamoja na mboga au kitoweo chochote ukipendacho. Ukiachana na nazi, pilau hii kama zilivyo pilau nyingine, hupikwa kwa kutumia viungo vya aina mbalimbali kama vile iliki na tangawizi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya nazi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Weka kikaango kwenye jiko lenye moto wa wastani. Weka ndani ya hicho kikaango, nazi iliyokunwa na uzikaange bila mafuta kwa lengo za kuzikausha, kwa muda wa dakika 1 mpaka 2, kisha epua na uweke pembeni.

    Step2

    Weka sufuria la ukubwa wa wastani lenye mafuta ya kupikia, kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka ndani ya hilo sufuria, mdalasini, karafuu pamoja na iliki, kisha kaanga kwa muda wa dakika 1. Weka vitunguu maji na ukaange kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona virunguu maji vimeiva.

    Step3

    Weka mchele na ukoroge vizuri. Weka tui la nazi, maji, pamoja na chumvi halafu koroga tena vizuri, kisha weka moto mkubwa na acha ichemke. Maji yakianza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika na acha ichemke kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona maji yote yaliyomo kwenye mchele yamekauka na wali umeiva. Hakikisha hugeuzi wali wakati unaupika.

    Step4

    Zima jiko, kisha epua wali na uweke pembeni. Acha wali utulie kwa muda wa dakika 5, kisha weka nazi iliyokunwa uliyo ikaanga, pamoja, giligilani na garam masala na ukoroge vizuri, kisha pakua kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.