Jarida la Mapishi

Mishikaki ya samaki

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 10
  • Walaji
    4

Mishikaki ya samaki, ni mishikaki mitamu inayopikwa kwa kuchanganya pamoja na viungo. Tofauti na mishikaki mingine, mishikaki hii kupikwa kwa kukaanga kwenye mafuta, badala ya kuoka kwenye moto. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mishikaki hii ya samaki.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya minofu ya samaki, chumvi, pamoja na binzari ya manjano, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka saa 2.

    Step3

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, unga wa mchele, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, pamoja na maji, kisha changanya vizuri.

    Step4

    Chukua vipande vya minofu ya samaki na uvipake mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha vipake unga wa mahindi.

    Step5

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango vipande vya minofu ya samaki ambayo vinatosha na kuenea kwenye kikaango, kisha kaanga huku ukivigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa vipande hivyo vya minofu ya samaki kutoka kwenye kikaango na uviweke kwenye kwenye chombo chenye paper towel ili vikauke mafuta, kabla ya kula. Rudia hatua hii kwa vipande vingine vyote vya minofu ya samaki vilivyobaki.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *