Jarida la Mapishi

Biriani ya nyama

Biriani ya nyama | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 25
  • Walaji
    4

Biriani ya nyama, ni chakula kitamu ambacho chafaa kuliwa hasa wakati wa sherehe. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia mchele, mtindi, viungo, pamoja na nyama ya aina yoyote ile; iwe ni nyama ya ng’ombe, au nyama ya mbuzi, au nyama ya kondoo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya nyama.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, korosho, vitunguu swaumu, tangawizi, majani ya giligilani, majani ya mvuje, nyanya, limao, garam masala, pamoja na 1½ vijiko vya chai vya chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step2

    Mimina mtindi ndani ya hilo kontena, kisha changanya vizuri.

    Step3

    Weka nyama, viazi mviringo, pamoja na matunda ya aprikoti, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vitu hivyo vimeenea vyema viungo. Funika kontena hilo vizuri, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.

    Step4

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step5

    Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.

    Step6

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step7

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona maji yote kwenye sufuria yamekauka ila wali haujaiva, kisha epua na uweke pembeni. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step8

    Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 230° C, kisha acha jiko lipate moto.

    Step9

    Chukua sufuria kubwa na ulipake siagi. Weka nusu ya wali ulio upika kwenye hilo sufuria, kisha sambaza vizuri.

    Step10

    Weka mchanganyiko wa nyama ulio uweka kwenye friji juu ya huo wali, kisha sambaza vizuri.

    Step11

    Weka nusu ya wali uliobaki juu ya huo mchanganyiko wa nyama, kisha sambaza vizuri.

    Step12

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, iliki, majani ya mbei, pamoja na binzari nyembamba halafu koroga vizuri, kisha zima jiko.

    Step13

    Mimina maziwa yenye zafarani halafu koroga vizuri, kisha epua na unyunyizie mchanganyiko huu juu ya wali.

    Step14

    Funika vizuri sufuria hilo kwa kutumia aluminium foil. Weka sufuria ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 15.

    Step15

    Punguza moto na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha endelea kuoka kwa muda wa saa 1, au hadi utakapo ona nyama imeiva na kuwa laini. Ondoa sufuria hilo kwenye jiko la kuoka na uliweke pembeni, kisha changanya biriani hiyo vizuri, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.