Jarida la Mapishi

Samaki wa kukaanga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Samaki wa kukaanga, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho huandaliwa kwa kuchanganya samaki pamoja na viungo, kisha kukaanga kwenye mafuta. Kitoweo hiki cha samaki wa kukaanga, chafaa kula pamoja na wali mweupe, wali wa binzari nyembamba, wali wa nazi, au wali wa ukwaju. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha samaki wa kukaanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, pilipili manga, garam masala, mbegu za kisibiti, chumvi, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na Tamarind Paste, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka minofu ya samaki, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona minofu yote ya samaki imeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka saa 4.

  Step3

  Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 1½ vya chakula vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto kwa muda wa dakika 2. Weka vipande vya minofu ya samaki ndani ya hicho kikaango, kisha kaanga kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona upande huo wa chini wa minofu umebadilika rangi na kuwa na rangi kahawia.

  Step4

  Nyunyizia mafuta ya kupikia yaliyobaki juu ya hiyo minofu ya samaki. Geuza vipande hivyo vya minofu ya samaki, kisha endelea kukaanga kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona upande huo wa minofu ulio geuza umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Epua vipande hivyo vya minofu ya samaki na uviweke kwenye sahani. Nyunyizia limao juu ya hiyo minofu ya samaki, kisha weka mezani tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *