Jarida la Mapishi

Wali mweupe

Wali mweupe | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Wali mweupe, ni chakula maarufu na kinacholiwa zaidi kuliko chakula cha aina yoyote duniani. Karibu nusu ya watu wote waliopo duniani, wanakula wali. Unaweza kupika wali huu kwa kutumia njia ya kuchemsha (boiling method), au kwa kutumia njia ya mvuke (steam method) ambayo ndio iliyo tumika kwenye pishi hili. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu mweupe.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step3

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step4

    Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.