![Garam masala | Jarida la Mapishi](https://www.jaridalamapishi.co.tz/wp-content/uploads/2023/06/garam_masala.jpg)
-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji1
Garam masala, ni mchanganyiko wa viungo ambao asili yake ni kutoka nchini India. Neno "Garam" lina maana ya moto na Neno "Masala" lina maana ya viungo mchanganyiko. Masala hii yafaa sana kutumika kwenye mchuzi au supu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeza garam masala hii kwa ajili ya kuiuza au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za shamari, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za pilipili manga, mbegu za iliki, pamoja na zafarani, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko ulio usaga kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke kwenye kontena safi.
Weka kwenye hilo kontena mdalasini, tangawizi, karafuu, basibasi, pamoja na kungumanga, kisha changanya vizuri.
Chukua mchanganyiko huo na urudishe kwenye kikaango, kisha kaanga tena kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 2 zaidi. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.
Mchanganyiko huo ukishapoa, uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye mapishi yako.
Leave a Review