Jarida la Mapishi

Achari ya minti

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Achari ya minti, ni achari yenye ladha nzuri ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani mabichi ya minti pamoja na viungo. Achari hii yafaa kula pamoja na kitafunio chochote kile ukipendacho, kama vile sambusa, sandwich, au chapati, fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika achari hii ya minti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, limao, pamoja na vijiko 2 vya chakula vya maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Weka majani ya minti pamoja na majani ya giligilani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Weka vijiko 2 vya chakula vya maji yaliyo bakia, mbegu za komamanga, pilipili manga, sukari, pamoja na chumvi, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

  Step4

  Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *