-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 55
-
Walaji4
Sosi ya nyanya na siagi, ni sosi tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia nyanya, siagi, heavy cream, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Sosi hii yafaa kula pamoja na wali, chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sosi hii ya nyanya na siagi.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye siagi na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi iyeyuke. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, majani ya mbei, iliki karafuu, vitunguu swaumu, pamoja na tangawizi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka nyanya, kungumanga, pamoja na maji, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva na kuwa laini, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko ulio upika, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na urudishe kwenye sufuria, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko lenye moto wa wastani.
Weka kwenye hilo sufuria, ½ kikombe cha maji, chumvi, pamoja na majani ya uwatu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Weka heavy cream halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5 zaidi. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review