Jarida la Mapishi

Achari ya nyanya

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 25
 • Walaji
  1

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za giligilani, mbegu za binzari nyembamba, choroko, dengu, pamoja na mbegu za pilipili manga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua sufuria ndogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, majani ya mvuje, vitunguu swaumu, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kaa muda wa sekunde kadhaa.

  Step3

  Weka mchanganyiko ulio usaga pamoja na chumvi, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 zaidi.

  Step4

  Punguza moto na uweke mdogo. Weka tomato sauce pamoja na Tamarind Paste, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona achari imekuwa nzito. Epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step5

  Hiifadhi achari hiyo kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *