Jarida la Mapishi

Achari ya vitunguu vya kijani na tangawizi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Achari ya vitunguu vya kijani na tangawizi, ni achari inayo tengenezwa kwa kusaga mchanganyiko wa vitunguu vya kijani, tangawizi, pamoja na viungo. Achari hii yafaa sana kutumika kwenye vitafunio vya vifungua kinywa, kama vile chapati wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya vitunguu vya kijani na tangawizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu vya kijani, limao, pamoja na mtindi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Weka sukari, chumvi, pamoja na majani ya minti, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *