-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji1
Achari ya minti na vitunguu swaumu, ni achari ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani mabichi ya minti, vitunguu swaumu, pamoja na viungo kama vile mbegu za haradali. Achari hii yafaa kutumia kwenye sambusa, sandwiches, chapati au mishikaki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya minti na vitunguu swaumu.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, karanga, vitunguu swaumu, pamoja na majani ya minti, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.
Weka Tamarind Paste, sukari, pamoja na chumvi, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.
Weka mchanganyiko ulio ukaanga kwenye mashine ya kusaga, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vizuri na kuwa laini.
Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.
Leave a Review