Jarida la Mapishi

Achari ya giligilani na limao

Achari ya giligilani na limao | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Achari ya giligilani na limao, ni achari tamu, ambayo hutengenezwa na kutumia majani mabichi ya giligilani, limao iliyo kamuliwa, pamoja na viungo. Achari hii yafaa kutumika kwenye sandwiches, sambusa, au kwenye kitafunio chochote kile ukipendacho. Pia unaweza kutumia achari hii kwenye nyama yoyote ile ya kuchoma. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza achari hii ya giligilani na limao.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka mbegu za binzari nyembamba ulizo zikaanga ndani ya hicho kinu, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimetwangika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, pilipili hoho, pamoja na vitunguu vya kijani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step4

    Weka majani ya giligilani, pamoja na majani ya minti, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

    Step5

    Weka limao, Chaat Masala, sukari, chumvi, pamoja na binzari nyembamba, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step6

    Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.