Jarida la Mapishi

Bisi za nanasi na pilipili

Bisi za nanasi na pilipili | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 1 Dk. 30
  • Walaji
    6

Bisi za nanasi na pilipili, ni bisi zenye ladha ya nanasi na pilipili zinazopikwa kwa kutumia tunda halisi la nanasi. Bisi hizi zafaa kula pamoja na kinywaji chochote cha baridi unacho kipenda. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika bisi hizi za nanasi na pilipili.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria ndogo na uiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani. Weka juisi ya nanasi kwenye hilo sufuria, halafu acha ichemke kwa muda wa saa 1, huku ukizungusha zungusha sufuria mara kwa mara, hadi utakapo ona juisi imekauka na kubakiwa na kijiko 1 tu chakula cha juisi ya nanasi katika sufuria, kisha epua na uweke pembeni.

    Step2

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, siagi, sukari, pilipili, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona sukari yote iliyomo kwenye kikaango imeyeyuka. Weka kijiko 1 chakula cha juisi ya limao iliyobaki kwenye kikaango kikubwa cha kwanza halafu koroga vizuri, kisha epua na uweke pembeni.

    Step3

    Washa jiko la kuoka (oven) na uweke joto la nyuzi 100° C, kisha acha jiko lipate moto.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa. Weka ndani ya hiyo sufuria, bisi pamoja na mchanganyiko uliomo kwenye kikaango kidogo, kisha changanya vizuri.

    Step5

    Weka sufuria hilo lenye mchanganyiko wa bisi kwenye jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 30.

    Step6

    Bisi zikisha iva, ziondoe kutoka kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe, kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.