Jarida la Mapishi

Kachori

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  N/A
 • Walaji
  4

Kachori, ni kitafunio ambacho asili yake kutoka katika nchi ya India. Kitafunio hiki hupikwa kwa kutumia viazi mviringo ambavyo hufinyangwa katika umbo la mpira na kuchanganywa pamoja na viungo, kisha kukaangwa. Fuata harua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kachori.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria. Weka ndani ya hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha vichemshe kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona viazi vimeiva. Viazi vikisha iva, mwaga maji yaliyomo ndani ya sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha viweke pembeni na uache vipoe. Menya viazi hivyo maganda yake yote, halafu viponde ponde.

  Step2

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, viazi mviringo ulivyo viponda, 1 kijiko cha chakula cha tangawizi, halafu changanya vizuri. Tumia mikono yako uliyokwisha nawa kwa maji safi na sabuni, kufinyanga mchanganyiko huo wa viazi mviringo na tangawizi, katika umbo la mipira midogo midogo, kisha weka viazi hivyo ulivyo vifinyanga kwenye sahani. Katika pishi hili, tarajia kupata viazi vyenye umbo la mipira kati ya 20 hadi 25.

  Step3

  Weka kikaango kwenye jiko lenye moto wa wastani. Weka vijiko viwili vya chakula vya mafuta ya kupikia, kisha acha yapate moto. Weka viazi ulivyo vifinyanga na uvikaange kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona viazi vimeiva. Wakati unakaanga viazi hivyo hakikisha huvikorogi, ila vigeuze kwa kutumia kijiko ikiwa utaona kuna haja ya kuvigeuza. Viazi vikisha iva, viondoe kwenye kikaango na uviweke kwenye kontena.

  Step4

  Weka kijiko 1 cha chakula kilichobakia cha mafuta ya kupikia, kwenye kikaango hicho hicho ulichotumia kukaanga viazi. Weka ½ kijiko cha chakula cha tangawizi pamoja na kijiko 1 cha chai cha vitunguu swaumu na pilipili ya kijani, kisha kaanga kwa muda wa dakika 1, huku ukikoroga mara kwa mara.

  Step5

  Weka nyanya ya kopo na upike kwa muda wa dakika 1 huku ukikoroga, kisha weka, limao, sukari pamoja na chumvi, halafu koroga vizuri. Weka viazi mviringo na upike kwa muda wa dakika 5 huku ukitikisa tikisa kikaango, ili kufanya viazi vichanganyike vyema pamoja na nyanya na viungo. Endelea kupika hadi utakapo ona mchanganyiko huo wa nyanya na viungo umekauka.

  Step6

  Weka vitunguu vya kijani na upike kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimeiva, kisha epua na uweke pembeni ili vipoe kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *