Jarida la Mapishi

Biskuti za kahawa na chocolate

Biskuti za kahawa na chocolate | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 48
  • Kupika
    Dakika 12
  • Walaji
    20

Biskuti za kahawa na chocolate, ni biskuti rahisi sana kupika ambazo hupikwa kwa kutumia unga halisi wa kahawa pamoja na chocolate. Biskuti hizi zafaa kuliwa pamoja na kikombe cha kahawa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za kahawa.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na dark chocolate. Chukua hilo bakuli na uliweke kwenye sufuria lenye maji moto, ili chocolate na siagi viyeyuke, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Chukua bakuli nyingine kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mayai na sukari halafu changanya vizuri, kisha weka kahawa na uendelee kuchanganya.

    Step3

    Mimina mchanganyiko wa chocolate na siagi na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 12, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.