Jarida la Mapishi

Biriani ya njugu

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Biriani ya njugu, ni chakula kitamu ambacho chafaa kuliwa hasa wakati wa sherehe. Chakula hiki hupikwa kwa kutumia mchele, maziwa, viungo, pamoja na mchanganyiko wa njugu za aina mbalimbali kama vile; lozi, pistachio, jozi, karanga, korosho na msonobari. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya njugu.

Bofya HAPA ili kujifunza jinsi ya kupika kaukau za tangawizi, ambazo utazitumia katika kupika biriani hii ya njugu.

Bofya HAPA ili kujifunza jinsi ya kupika kaukau za vitunguu maji, ambazo utazitumia katika kupika biriani hii ya njugu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua sufuria kubwa lenye kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mchanganyiko wa njugu pamoja na zabibu kavu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3, au hadi utakapo ona njugu zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mchanganyiko huo kwenye sufuria na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step3

  Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Weka kwenye sufuria hilo hilo kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia yaliyobaki, kisha acha mafuta yapate moto. Weka garam masala pamoja na mchele, kisha kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona mchele umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step4

  Weka maji pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke.

  Step5

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona maji yote kwenye sufuria yamekauka ila wali haujaiva, kisha epua na uweke pembeni. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step6

  Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto.

  Step7

  Chukua sufuria kubwa na ulipake siagi. Weka nusu ya wali ulio upika kwenye hilo sufuria, kisha sambaza vizuri.

  Step8

  Weka mchanganyiko wa njugu ulioupika juu ya huo wali, kisha sambaza vizuri.

  Step9

  Weka nusu ya wali uliobaki juu ya huo mchanganyiko wa njugu, kisha sambaza vizuri.

  Step10

  Nyunyizia maziwa yenye zafarani juu ya huo wali.

  Step11

  Weka kaukau za vitunguu maji pamoja na kaukau za tangawizi, kisha sambaza vizuri.

  Step12

  Funika vizuri sufuria hilo kwa kutumia aluminium foil. Weka sufuria ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona biriani imeiva. Ondoa sufuria hilo kwenye jiko la kuoka na uliweke pembeni.

  Step13

  Nyunyizia binzari nyembamba kwenye hilo sufuria lenye biriani, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *