Jarida la Mapishi

Pilau ya haradali

Pilau ya haradali | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Pilau ya haradali, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, majani ya minti, majani ya mvuje, pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile; mbegu za haradali, pilipili manga na binzari nyembamba. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya haradali.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za haradali, pilipili manga, mbegu za uwatu, majani ya mvuje, majani ya minti, pamoja na majani ya uwatu, kisha koroga vizuri.

    Step3

    Weka mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele.

    Step4

    Weka chumvi pamoja na binzari ya manjano, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step5

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step6

    Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.