Jarida la Mapishi

Kaukau za vitunguu maji

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  1

Kaukau za vitunguu maji, ni viungo ambavyo hutengenezwa kwa kukaanga vitunguu maji vilivyo katwa katwa kwenye mafuta. Kaukau hizi hutumika kwenye chakula kama viungo vya kupendezesha au kuongeza ladha kwenye chakula, hasa kwenye mchuzi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kaukau hizi za vitunguu maji.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka nusu ya vitunguu maji ulivyo vikata kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa vitunguu hivyo kwenye kikaango na uviweke pembeni kwenye kontena lenye paper towel, kisha acha vipoe. Rudia hatua hii kwa nusu ya vitunguu maji vilivyobaki.

  Step2

  Weka viungo hivyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi kwenye friji.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *