Jarida la Mapishi

Kuku wa giligilani na apple

Kuku wa giligilani na apple | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    4

Kuku wa giligilani na apple, ni kitoweo chenye ladha nzuri ambacho hupikwa kwa kutumia kuku, majani ya giligilani yaliyo katwa, matunda ya apple yaliyo katwa katwa, pamoja na viungo vya aina mbali mbali kama vile; vitunguu swaumu na tangawizi. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja ma wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa giligilani na apple.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku, tangawizi, vitunguu swaumu, limao, mtindi, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimechanganyika vyema pamoja na viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka 24.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step3

    Weka vitunguu maji pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step4

    Weka vipande vya nyama ya kuku pamoja na mchanganyiko wake wote wa viungo, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

    Step5

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, majani ya giligilani pamoja na apple, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step6

    Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa kuku, kisha pika mchanganyiko huo huku ukivigeuza vipande vya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 25, au hadi utakapo ona vipande hivyo vya nyama ya kuku vimeiva.

    Step7

    Weka garam masala, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.