Jarida la Mapishi

Achari ya dengu na karanga

Achari ya dengu na karanga | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga dengu pamoja na karanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye bakuli safi.

  Step2

  Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, majani ya giligilani pamoja na limao, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Weka mchanganyiko wa dengu ulio usaga mwanzoni, sukari, pamoja na chumvi, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

  Step4

  Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.