Jarida la Mapishi

Achari ya ufuta na karanga

Achari ya ufuta na karanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za ufuta mweupe kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua na uweke pembeni ili zipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za ufuta mweupe ulizo zikaanga, maji ya moto, majani ya giligilani, karanga, Tamarind Paste, vitunguu swaumu, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utalapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, kisha uhifadhi kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.