-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji1
Chaat masala, ni mchanganyiko wa viungo ambao hutengenezwa kwa kutumia mango powder kama kikuu pamoja na viungo vingine. Chaat Masala yafaa kutumia kwenye saladi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeza chaat masala hii kwa ajili ya kuiuza, au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mango powder, binzari nyembamba, citric acid, black salt, chumvi, mbegu za kisibiti, tamarind powder, pamoja na majani ya minti, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Weka viungo hivyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi mahali pakavu penye baridi.
Leave a Review