-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji1
Sosi ya ukwaju (Tamarind Paste), ni sosi yenye mchanganyiko wa ladha ya utamu na uchachu, ambayo hutengenezwa kuroweka ukwaju kwenye maji ya moto. Sosi hii hutumika kuongeza ladha kwenye vyakula vya aina mbali mbali, kama vile nyama, saladi, wali, mboga, n.k. Fuata hatua zufuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza sosi hii ya ukwaju.
Ingredients
Directions
Chukua kontena. Weka kikombe 1 cha maji, kisha roweka ukwaju ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa saa 1 mpaka 2.
Chukua ukwaju ulio uroweka na usugue taratibu kwa kutumia mikono, hadi utakapo ona ukwaju wote umetoka na kubakiwa na mbegu peke yake, kisha zitupe hizo mbegu.
Chuja kwenye bakuli mchanganyiko huo wa ukwaju kwa kutumia chujio, kisha rudisha machicha yake kwenye kontena.
Weka ½ kikombe cha maji yaliyobaki kwenye hilo kontena, kisha sugua tena mchanganyiko huo taratibu kwa kutumia mikono.
Chuja tena mchanganyiko huo wa ukwaju kwa kutumia chujio kwenye bakuli lile lile, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo wote wa ukwaju.
Hifadhi sosi hii ya ukwaju kwenye chombo chenye mfuniko na kutumia kidogo kidogo kwenye chakula cha aina yoyote ile.
Leave a Review