Jarida la Mapishi

Sosi ya nyanya na ukwaju

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Sosi ya nyanya na ukwaju, ni sosi nzuri yenye ladha ya mchanganyiko wa utamu na uchachu ambao unatokana na nyanya, ukwaju, pamoja na viungo. Sosi hii yafaa sana kula pamoja na wali au pamoja na chakula chochote kile ukipendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sosi hii ya nyanya na ukwaju.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani kisha acha kikaango kipate moto. Weka karanga kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step2

  Weka kwenye kikaango hicho hicho, nazi, mbegu za giligilani, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za mpopi, pamoja na mbegu za ufuta, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2. Epua na uweke pembeni kwenye kontena lenye karanga, kisha acha vipoe.

  Step3

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko wa karanga na viungo ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Weka binzari ya manjano, kisha saga tena hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

  Step5

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za haradali, black seeds, nyanya, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, chumvi, pamoja na mchanganyiko wa karanga na viungo ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 13 mpaka 15, au hadi utakapo ona nyanya zimeiva na kuwa laini.

  Step6

  Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka Tamarind Paste, kisha endelea kupika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 30 (Kumbuka kukoroga mara 1 au 2, wakati unapika).

  Step7

  Epua sosi hiyo na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *