Jarida la Mapishi

Biskuti za apple

 • Maandalizi
  Saa 1
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  20

Biskuti za apple, ni biskuti tamu ambazo zafaa kuliwa hasa katika msimu wa vuli. Biskuti hizi hupikwa kwa kutumia matunda halisi ya apple ambayo hufanya biskuti hizi ziwe tamu zaidi na laini. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za apple.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mafuta ya nazi, sukari, pamoja na yai, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka maji na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, chumvi, baking powder, mdalasini, na matunda ya apple, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *