Jarida la Mapishi

Sambusa za njegere

Sambusa za njegere | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Saa 2 Dk. 15
  • Walaji
    24

Sambusa za njegere, ni sambusa tamu ambazo zinawafaa hasa wale ambao hawapendi kula sambusa zenye nyama. Sambusa hizi hupikwa kwa kutumia njegere pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika sambusa hizi za njegere.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria dogo lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step2

    Weka njegere, mbegu za giligilani, tangawizi, mbegu za shamari, pilipili ya unga, pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step3

    Mimina kikombe 1 cha maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step4

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona njegere zimeiva.

    Step5

    Weka mango powder halafu koroga vizuri, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step6

    Chukua mashine ya kusaga (food processor). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vikombe 1½ vya unga wa ngano, baking powder, chumvi, baking soda, ¼ kikombe cha mafuta ya kupikia, mbegu za kisibiti, pamoja na kijiko 1 cha chai cha chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.

    Step7

    Mimina ⅓ ya kikombe cha maji taratibu wakati mashine ikiendelea kuzunguka, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umejikusanya na kuwa donge lenye umbo la mpira ambalo halishikamani na chombo. Ondoa donge hilo kutoka kwenye mashine ya kusaga na uliweke kwenye kontena. Funika vizuri kontena hilo, kisha acha donge liumuke kwa muda wa saa 1 mpaka saa 4.

    Step8

    Chukua mafuta ya kupikia kiasi na uyapake kwenye viganja vya mikono yako. Chukua donge lililomo kwenye kontena, kisha ligawe katika madonge 12 ya maumbo ya mpira yenye uwiano unao fanana. Weka madonge hayo kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo.

    Step9

    Chukua kibao cha kusukumia chapati. Chukua donge moja kutoka kwenye kontena na uliweke juu ya kibao cha kusukumia chapati, kisha kandamiza vizuri donge hilo kwa kutumia kiganja cha mkono wako hadi utakapo ona imekuwa bapa.

    Step10

    Chukua unga wa ngano na upake juu ya donge ulilo likandamiza. Chukua kifimbo cha kusukumia chapati, kisha sukuma hadi utakapopata chapati ya upana wa kati ya nchi 6 hadi 7. (Unaweza kupaka unga zaidi wakati unasukuma, ikiwa utaona donge hilo linanata)

    Step11

    Chukua kisu na ukate chapati hiyo katikati, kisha chukua maji na upake kwenye kingo za vipande hivyo vya chapati.

    Step12

    Chukua kipande kimoja cha chapati. Chukua upande mmoja wa kipande hicho cha chapati na ukunje katikati, halafu chukua na upande wa pili wa kipande hicho cha chapati na ukunje pia katikati ili kutengeneza umbo la koni. Hakikisha kingo za pande zote mbili za hiyo chapati zimekutana, kisha kandamiza kingo hizo ili ziweze kushikamana.

    Step13

    Fungua mdomo wa koni hiyo ya sambusa, kisha weka ndani yake vijiko 2 hadi 3 vya chakula vya mchanganyiko wa sambusa ulio upika.

    Step14

    Chukua maji na upake kwenye kingo za mdomo wa koni hiyo ya sambusa, kisha kandamiza kingo hizo, hadi utakapo ona mdomo wa sambusa umejifunga vizuri. Weka sambusa hiyo kwenye kontena safi, kisha funika vizuri kontena hilo, hadi utakapokuwa tayari kukaanga sambusa hizo. Rudia hatua ya 4 hadi ya 7 kwa madonge yaliyobaki.

    Step15

    Chukua kikaango kikubwa chenye vikombe 2 vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango sambusa ambazo zinatosha na kuenea kwenye kikaango, kisha kaanga huku ukizigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa sambusa hizo kutoka kwenye kikaango na uziweke kwenye kwenye chombo chenye paper towel ili zikauke mafuta, kabla ya kula. Rudia hatua hii kwa sambusa nyingine zote zilizobaki.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.