Jarida la Mapishi

Ice cream ya karanga

Ice cream ya karanga | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 35
  • Kupika
    -
  • Walaji
    3

Ice cream ya karanga, ni ice cream ambayo hutengenezwa kwa kutumia siagi ya karanga pamoja na krimu. Ice cream hii yafaa sana kuliwa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya karanga.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua ganda la vanilla na ulikate, kisha ondoa mbegu zilizomo kwenye hilo ganda.

    Step2

    Chukua sufuria ndogo. Weka ndani ya hilo sufuria, maziwa, double cream, pamoja na mbegu za vanilla, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani huku ukikoroga. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5, kisha epua na uweke pembeni.

    Step3

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli mayai pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa maziwa ulio chemsha, kisha koroga vizuri.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa. Weka maji ya moto kwenye hilo sufuria. Weka mchanganyiko wa maziwa ulio uchemsha ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha changanya kwa kupiga piga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

    Step5

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli maji ya baridi pamoja na vipande vya barafu (ice cubes). Ondoa sufuria ndogo ulilo liweka ndani ya sufuria kubwa lenye maji ya moto, halafu weka sufuria hilo ndani ya bakuli lenye maji ya baridi, kisha koroga vizuri mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

    Step6

    Weka siagi ya karanga na unachanganye vizuri, kisha ondoa sufuria hilo lenye mchanganyiko wa ice cream kutoka kwenye bakuli lenye maji baridi, kisha mimina mchanganyiko huo kwenye kontena. Funika vizuri kontena hilo halafu liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1.

    Step7

    Baada ya saa 1, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step8

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.