Jarida la Mapishi

Keki ya buttermilk na chocolate

Keki ya buttermilk na chocolate | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    10

Keki ya buttermilk na chocolate, ni keki tamu yenye harufu nzuri ya kuvutia. Keki hii hupikwa kwa kutumia maziwa ya buttermilk pamoja na chocolate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya buttermilk na chocolate.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli la kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking powder, cocoa powder, chumvi, siagi, sukari, vanilla extract, mayai, pamoja na buttermilk, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step2

    Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

    Step3

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.