Jarida la Mapishi

Cupcakes za ufuta

Cupcakes za ufuta | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 1 Dk. 5
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    14

Cupcakes za ufuta, ni cupcakes ambazo hupikwa kwa kutumia unga wa ngano, mbegu za ufuta, pamoja na mayai. Cupcakes hizi zafaa kula kama kitindamlo, wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika cupcakes hizi za ufuta.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka mayai, maziwa na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Weka unga wa ngano, unga wa ufuta mweusi, chumvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20 mpaka 25, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.