Jarida la Mapishi

Keki ya strawberry na limao

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  10

Keki ya strawberry na limao, ni keki tamu inayopikwa kwa kutumia matunda ya strawberry yaliyo katwa katwa, limao iliyo kamuliwa pamoja na maganda ya limao yaliyokunwa. Keki hii yafaa sana kula katika kipindi cha kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya strawberry na limao.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mayai, olive oil, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka maganga ya limao yaliyo kunwa na limao iliyo kamuliwa, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, baking powder, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *