Jarida la Mapishi

Ice cream ya vanilla

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  -
 • Walaji
  3

Ice cream ya vanilla, ni ice cream tamu inayo tengenezwa kwa kutumia mmea wa vanilla, maziwa, pamoja na krimu. Ice cream hii yaweza kuliwa kama kitindamlo, wakati wowote ule uupendao. Fuata haua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya vanilla.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua ganda lenye mbegu za vanilla. Kata ganda hilo na uondoe mbegu za vanilla.

  Step2

  Chukua sufuria ndogo. Weka ndani ya hilo sufuria, maziwa, double cream, pamoja na mbegu za vanilla, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto mdogo kwa muda wa dakika 5, huku ukikoroga mara kwa mara.

  Step3

  Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, viini vya mayai pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa maziwa, halafu koroga vizuri.

  Step4

  Chukua sufuria kubwa. Weka maji ya moto kwenye hilo sufuria. Weka mchanganyiko wa maziwa ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha changanya kwa kupiga piga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

  Step5

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli maji ya baridi pamoja na vipande vya barafu (ice cubes). Ondoa sufuria ndogo ulilo liweka ndani ya sufuria kubwa lenye maji ya moto, halafu weka sufuria hilo ndani ya hili bakuli lenye maji ya baridi, kisha koroga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

  Step6

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko wa maziwa, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 8.

  Step7

  Baada ya saa 8, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step8

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *