Jarida la Mapishi

Cupcakes za parachichi na chocolate

 • Maandalizi
  Saa 1 Dk. 10
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  12

Cupcakes za parachichi na chocolate, ni cupcakes tamu ambazo zinawafaa watu ambao wanapendelea kula vyakula vya mboga. Cupcakes hizi zaweza kuliwa kama kitindamlo kwenye mlo wowote ule, au katika sherehe. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika cupcakes hizi za parachichi na chocolate.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, parachichi, light brown sugar, tui la nazi, vanilla extract, yai, pamoja na ute wa mayai, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka unga wa ngano ambao hauja kobolewa, unga wa ngano, chumvi, baking powder, pamoja na cocoa powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *