Jarida la Mapishi

Pilau ya kuku

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Pilau ya kuku, ni chakula maarufu katika Mataifa ya India, Ulaya, Urusi, Iran na Afrika Mashariki. Chakula hiki hupikwa kwa kuchanganya wali, nyama ya kuku pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya kuku.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli au kontena la ukubwa wastani. Weka ndani ya hilo bakuli maji pamoja na mchele na uroweke kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Weka sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia, kwenye jiko lenye moto wa mkubwa. Weka iliki pamoja na mdalasini, kisha kaanga kwa muda wa sekunde 30. Weka vitunguu maji na ukaange kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

  Step3

  Weka vitunguu swaumu pamoja na tangawizi, na ukaange kwa muda wa dakika 1. Weka giligilani, binzari nyembamba, majani makavu ya uwatu, garam masala, binzari ya manjano pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, na uendelee kukaanga kwa muda wa dakika 1.

  Step4

  Weka kuku pamoja na nyanya, kisha koroga vizuri. Mimima mtindi kisha koroga, hadi utakapo ona maziwa yameanza kuchemka. Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache kuku achemke kwa muda wa dakika 10 hadi 15, au hadi utakapo ona kuku ameiva, na mchuzi umekuwa mzito. Ondoa vipande hivyo vya kuku na uviweke kwenye konena au bakuli safi na ubakize mchuzi peke yake ndani ya sufuria.

  Step5

  Weka mchele kwenye hilo sufuria lenye mchuzi na ukoroge vizuri, kisha weka maji pamoja na ½ kijiko cha cha chumvi kilicho bakia, halafu koroga vizuri. Ongeza moto na uweke moto mkubwa kisha acha wali uchemke. Maji yakianza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na acha wali uendelee kuchemka kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona maji yaliyomo kwenye sufuria yamekauka.

  Step6

  Weka kuku kwenye sufuria lenye wali na uchanganye vizuri, kisha funika sufuria na upike wali kwa muda wa dakika 10 mpaka 12 au hadi utakapo ona wali umeiva.

  Step7

  Wali ukishaiva, zima jiko na uache hilo sufuria lenye pilau juu ya jiko kwa muda wa dakika 5, kabla ya kupakua.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *