Jarida la Mapishi

Wali wa biringanya

Wali wa biringanya | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Wali wa biringanya, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia wali mweupe ambao huchanganywa pamoja na biringanya na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa biringanya.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, nazi, mbegu za giligilani, choroko, dengu, binzari nyembamba, mbegu za ufuta, iliki, pamoja na pilipili manga, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko ulio ukaanga kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Weka binzari ya manjano, karafuu, pamoja na mdalasini, kisha saga tena hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwemye hilo sufuria, mbegu za haradali, majani ya mvuje, biringanya, chumvi, pamoja na ½ ya mchanganyiko ulio usaga, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 12 mpaka 13, au hadi utakapo ona biringanya zimeiva na kuwa laini.

    Step5

    Weka Tamarind Paste halafu koroga vizuri, kisha pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 5.

    Step6

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka wali mweupe uliopikwa pamoja na ½ viungo ulivyo visaga vilivyobaki, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na upike wali huo kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

    Step7

    Epua wali huo na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.