Jarida la Mapishi

Pilau ya vitunguu na brokoli

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 25
 • Walaji
  4

Pilau ya vitunguu na brokoli, ni chakula kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, mboga ya brokoli, vitunguu maji, pamoja na viungo vya aina mbali mbali kama vile; iliki, mdalasini, pamoja na karafuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya vitunguu na brokoli.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani lenye vijiko 3 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, iliki, mdalasini, pamoja na karafuu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.

  Step3

  Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step4

  Nyunyizia sukari juu ya hivyo vitunguu, kisha endelea kukaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona vitunguu hivyo vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia iliyokolea.

  Step5

  Weka mchele pamoja na maji uliyotumia kurowekea mchele, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step6

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step7

  Wali ukishaiva zima jiko na uache utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko.

  Step8

  Chukua sufuria ndogo lenye kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria binzari nyembamba, mbegu za haradali, pamoja na brokoli, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni.

  Step9

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena wali ulio upika pamoja na mchanganyiko wa brokoli, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *