Jarida la Mapishi

Wali wa ufuta

Wali wa ufuta | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Wali wa ufuta, ni wali wenye ladha nzuri na rahisi kupika, ulio sheheni madini mengi ya chuma. Wali huu wafaa kuliwa pamoja na mboga za majani, saladi au mtindi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa ufuta.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, mchele, maji, pamoja na chumvi, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

    Step2

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step3

    Zima jiko, kisha acha wali utulie kwa muda wa dakika 5, ukiwa bado juu ya jiko.

    Step4

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za ufuta mweupe kwenye hicho kikaango, kisha kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mbegu hizo za ufuta mweupe kwenye kikaango na uziweke kwenye kontena.

    Step5

    Weka choroko kwenye kikaango hicho hicho, kisha, halafu kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step6

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, choroko pamoja na mbegu za ufuta, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vuzuri na kuwa laini.

    Step7

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, korosho pamoja na majani ya mvuje, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step8

    Weka vitunguu vya kijani, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30 zaidi, kisha epua na umimine kwenye sufuria lenye wali.

    Step9

    Weka pia mchanganyiko wa ufuta mweupe ulio usaga kwenye huo wali, kisha changanya vizuri.

    Step10

    Chukua sufuria lenye wali na uliweke kwenye jiko lenye moto mdogo, halafu funika sufuria na upike kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.