Jarida la Mapishi

Pilau ya nyama

Pilau ya nyama | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 50
  • Walaji
    4

Pilau ya nyama, ni chakula cha kipekee na maarufu ambacho hupendwa kuliwa kwenye sherehe, na hakiwezi kukosekana kwenye sherehe yoyote ile. Chakula hiki cha pilau ya nyama, waweza kukipika kwa kutumia nyama yoyote ile, iwe ya nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi au nyama ya kondoo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya nyama.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30. Baada ya dakika 30, hifadhi vikombe 1¼ vya maji uliyotumia kurowekea mchele, kisha mwaga maji mengine yote yaliyobaki.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step3

    Weka nyama, tangawizi, vitunguu swaumu, nyanya, mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 23 mpaka 25, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Weka viazi mviringo, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step5

    Weka mchele, vikombe 1¼ vya maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na maziwa halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step6

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali, nyama, pamoja na viazi vimeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

    Step7

    Nyunyizia iliki na ukoroge vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Recipe Reviews

    Avarage Rating:
    • 5 / 5
    Total Reviews:( 1 )
    • Rehema

      Thanks

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.