Jarida la Mapishi

Mchuzi wa samaki

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  4

Mchuzi wa samaki, ni kitoweo kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia samaki wabichi, vitunguu, nyanya, tui la nazi pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa samaki.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mbegu za giligilani, mbegu za haradali, pamoja na mbegu za pilipili manga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kutoka kwenye mashine ya kusaga, na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step2

  Weke kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, ½ ya vitunguu maji ulivyo vikata pamoja na vitunguu swaumu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Weka mchanganyiko wa viungo ulio usaga mwanzoni, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha saga tena hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

  Step4

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, minofu ya samaki, pamoja na mchanganyiko wa viungo ulio usaga, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya minofu ya samaki vimechanganyika vyema pamoja na mchanganyiko wa viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 1 mpaka 4.

  Step5

  Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 1½ vya chakula vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye kwenye hicho kikaango, ½ ya vitunguu maji vilivyobaki pamoja na tangawizi, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.

  Step6

  Weka vijiko 1½ vya chakula vya mafuta ya kupikia yaliyobaki kwenye hicho hicho kikaango, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vipande vya minofu ya samaki, kisha kaanga kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Kumbuka kugeuza vipande hivyo vya minofu ya samaki mara 1 au 2 wakati unakaanga.

  Step7

  Mimina tui la nazi, kisha weka moto mdogo na uache ichemke kwa muda wa dakika 5. Hakikisha hukorogi kabisa wakati inachemka.

  Step8

  Weka white vinegar na ukoroge vizuri, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 2 mpaka 3 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *