Jarida la Mapishi

Wali wa kukaanga wa nyama ya nguruwe

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 15
 • Walaji
  4

Wali wa kukaanga wa nyama ya nguruwe, ni pishi zuri linalopikwa kwa kutumia wali, nanasi, nyama ya nguruwe tangawizi, karoti pamoja na majani ya figili. Mchanganyiko wa mahitaji haya hufanya chakula hiki kiwe cha kuvutia na chenye ladha nzuri. Ikiwa wewe ni mpenzi wa wali wa kukaanga, basi nakuhakikishia utakipenda chakula hiki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika wali huu wa kukaanga wa nyama ya nguruwe.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa chenye vijiko 2 vya chai vya mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka nyama ya nguruwe kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5. Ondoa nyama ya nguruwe kwenye kikaango na uiweke kwenye sahani.

  Step2

  Weka kijiko 1 cha chakula cha mafuta ya kupikia kwenye kikaango hicho hicho, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu vya kijani, vitunguu swaumu, mboga ya figili, tangawizi, karoti, pamoja na vipande vya nanasi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4 mpaka 5.

  Step3

  Chukua bakuli. Weka ndani ya hilo bakuli, ute wa mayai 2 pamoja yai 1 zima, halafu piga piga mayai hayo vizuri, kisha mimina kwenye kikaango na uache yaive upande wa chini.

  Step4

  Weka wali mweupe, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2.

  Step5

  Weka nyama ya nguruwe uliyo ikaanga, njegere, soy sauce, pamoja na majani ya giligilani, halafu changanya vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *