Jarida la Mapishi

Pilau ya maharage ya soya

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  Dakika 30
 • Walaji
  4

Pilau ya maharage ya soya, ni chakula kizuri na chenye afya ambacho hupikwa kwa kutumia mchele, pilipili hoho, nyanya, maharage ya soya, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika pilau hii ya maharage ya soya.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka maji, kisha roweka mchele ndani ya hilo kontena lenye maji kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, mbegu za uwatu, vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, maharage ya soya, nyanya, garam masala, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.

  Step3

  Weka mchele, maji uliyotumia kurowekea mchele, pamoja na pilipili hoho halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

  Step4

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka taratibu kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona wali umeiva na maji yote kwenye sufuria yamekauka. Hakikisha hukorogi kabisa wali wakati unaupika.

  Step5

  Zima jiko, kisha acha pilau itulie kwa muda wa dakika 5, ikiwa bado juu ya jiko. Baada ya dakika 5, pakua pilau kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *